Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Ibrahim al-Zaben, Balozi wa Palestina nchini Brazili na mwakilishi kwa wakati mmoja nchini Paraguay, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari vya kikanda, alisisitiza:
“Wananchi wa Palestina, waliomo ndani na nje ya ardhi ya asili yao, kwa shauku kubwa wanakaribisha kuongezeka kwa utambuzi wa kimataifa wa taifa la Palestina. Utambuzi huu si zawadi au upendeleo, bali ni utekelezaji wa haki ya kihistoria, kisheria na kimaadili kwa watu waliopigania zaidi ya miongo saba kwa ajili ya uhuru, kujitegemea na mamlaka juu ya ardhi yao.”
Aliongeza kuwa: “Mchakato huu unaakisi irada ya jumuiya ya kimataifa katika kulinda sheria za kimataifa na maazimio halali ya kimataifa, na unaonyesha kwamba kuendelea kwa ubeberu wa Israel ndicho kizuizi kikuu cha kupatikana kwa amani na usalama katika eneo na ulimwengu mzima.”
Ubalozi wa Palestina katika taarifa yake ulisisitiza kuwa: “Watu wa Palestina wamesalia thabiti katika kujitolea kwao kwa amani ya haki na ya kina, kwa msingi wa sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa, na wanakataa uvamizi, ujenzi wa vitongoji na uchokozi katika hali yoyote ile. Mataifa hayawezi kufutwa, haki haziwezi kufutika, na irada ya uhuru daima ni yenye nguvu kuliko nguvu yoyote ya.”
Al-Zaben, mwishoni, huku akitoa wito maalumu kwa serikali ya Paraguay, alibainisha kuwa: “Kushiriki kwa Paraguay katika mchakato wa kimataifa wa kulitambua taifa la Palestina kutakuwa na mchango wenye thamani katika kujenga mustakabali unaojengwa juu ya kuishi kwa amani na kuheshimiana baina ya mataifa. Utambuzi wa taifa la Palestina ni uwekezaji katika mustakabali unaojengwa juu ya amani ya haki; njia salama ya kujenga ulimwengu thabiti, salama na usio na vurugu na misimamo mikali ambayo ubeberu huzalisha.”
Maoni yako